Na Zainab Nyamka  Globu ya Jamii

Kampuni ya simu ya Airtel sambamba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Jamal Malinzi wamewataka wadau kujitokeza kuisapoti timu ya vijana ya chini ya miaka 17 Serengeti Boys ambao wamefanikiwa kwenda kombe la Mataifa Afrika kwa vijana (AFCON) nchini Gabon mwezi Mei mwaka huu.

Malinzi alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupata nafasi ya ushiriki kwa vijana hao baada ya timu ya Congo Brazaville kushindwa kumpelekea mchezaji wao Langa ambae alisadikiwa kuwa na umri mkubwa zaidi na kuchezeshwa kwenye mashindano ya vijana.

Malinzi amewataka wadau kwa pamoja kusaidiana nao katika kuaindaa timu ya vijana kwani hakika mashindano haya yanahitaji kiasi kikubwa cha fedha takribani dola laki tano (500,000) ili timu iweze kuweka kambi nje ya nchi na hata kupata vifaa vya kutosha na vya kisasa.

Meneja wa Mawasiliano  Airtel, Jackson Mmbando amesema kuwa wanawapongeza TFF kwa hatua kubwa waliyofikia ya kuifikisha hapa Serengeti Boys ila bado vijana hawa wanahitaji kupata sapoti kutoka kwa wadau na seriakali kwa ujumla.

Mmbando amesema kuwa,  vijana hawa wanahitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi na kujengwa kisaikolojia ili waweze kufanya vizuri kwani waliona walishaondolewa  kwenye michuano hiyo.

"Vijana hawa wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau ili waweze kufanikisha safari yao ya Gabon mwezi wa tano na sisi kama airtel tutasaidia katika kuitangaza timu hiyo,"amesema Mmbando

Airtel wamekuwa wadau wakubwa sana wa kukuza soka la vijana kwa kuanzisha mashindano ya Airtel Rising Star ambapo hivi karibuni waliweza kufanya usaili wa vijana na wengine wakiwa tayari kwenye kikosi cha vijana wa Serengeti Boys.
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kufuzu kwa Serengeti kwenda Mataifa Afrika kwa vijana nchini Gabon, Kulia ni Meneja Mahusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Meneja wa Mahusiano Airtel Jackson Mmbando akizungumza na waandishi na kuwataka wadau kujitokeza kuisapoti Serengeti Boys ili waweze kufanya vizuri kwa mashindano ya Mataifa Afrika kwa Vijana nchini Gabon

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...