JE, UNATUMIA JIKO LA GESI KUPIKIA SOMA HII
MUHIMU.
... na uchukue tahadhari ili isitokee
kwako. Hili linaweza kuwa ni kosa la kawaida katika kila nyumba.
JINSI ILIVYOTOKEA
Jiko la gas lilikuwa linamewaka na mapishi
yakiendelea.
Mama akaona mende jirani na sink la
kuoshea vyombo. Mara akachukua kopo la dawa ya mbu na kupuliza karibu na
lile jiko la gas linalowaka.Ulitoka mlipuko mkubwa na ndani ya muda mfupi yule
mama alikuwa ameungua kwa asilimia 65.
Mumewe alikimbilia kuuzima ule moto na
nguo zake nazo zilishika moto.Mumewe bado yuko hospitali akiuguza majeraha ya
moto na bado hana habari kwamba mke wake alifariki alipofikishwa tu hospitali.
Ni vema tukafahamu kuwa dawa zote za
kuulia wadudu "Hit", "Marten", "heaven",
"Raid" n.k. zina mchanganyiko wa madawa mengi yanayosababisha mlipuko
mkubwa.Mchanganyiko huu wa madawa ni rahisi sana kusababisha mlipuko haraka
sana. Tafadhali elimisha wanafamilia yako na rafiki zako kuhusu jambo hili,
kwani yeyote yanaweza kumtokea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...