Ndugu Wananchi,

Tarehe 3 Machi kila mwaka watanzania wote huungana na nchi nyingine za Afrika katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Afrika, ambayo huadhimishwa barani Afrika kila mwaka. Siku hii imetengwa kwa lengo la kukumbuka umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira barani Afrika. 

Azimio la kuadhimisha Siku hii lilipitishwa na kuamuliwa na Baraza la Mawaziri wanaosimamia Mazingira wa nchi za Afrika kwenye mkutano uliofanyika Durban, Afrika Kusini Mwaka 2002. Siku hii iliamuliwa iwe kielelezo cha kukuza weledi kuhusu kupambana na uharibifu wa mazingira pamoja na kuenea kwa hali ya jangwa Afrika. Kuanzia wakati huo siku hii ilikuwa inaadhimishwa nchini Ethiopia kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Ndugu Wananchi,

Kikao cha 12 cha Baraza la Mawaziri wa Mazingira (AMCEN) kiliamua kwamba maadhimisho ya siku hii yawe yanafanyika kikanda. Hivyo kuanzia mwaka 2009 maadhimisho ya siku ya Mazingira Afrika yalianza kufanyika kikanda katika nchi za Afrika na ndipo, mwaka 2010 nchi yetu ikapata fursa ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya yaliyofanyika jijini Arusha. 

Aidha, Umoja wa Afrika kwa kutambua juhudi na kazi iliyofanywa na Prof. Wangari Maathai kutokana na mchango wa mwanamke huyu katika hifadhi ya mazingira na kuwezesha wanawake katika usimamizi endelevu wa maliasili na mazingira kwa ujumla waliamua tarehe 3 Machi kila mwaka iwe pia ni siku ya kumkumbuka yake iende sambamba na maadhimisho ya siku ya Mazingira Afrika. Hivyo tangu mwaka 2012 maadhimisho ya Siku ya Mazingira Afrika yamekuwa yakienda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wangari Maathai ili kutambua mchango wake katika utunzaji wa Mazingira. Mwanamke huyu alipata Tuzo ya heshima ya Nobel Laureate’s green legacy kutokana na juhudi alizofanya. 
Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora, akitoa Tamko la Siku ya Mazingira Afrika kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Mkamba, Leo katika mkutano na waandishi wa Habari Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira wa Ofisi hiyo Bw. Richard Muyungi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...