WANACHAMA wa mfuko wa pensheni wa PSPF sasa wataanza kupata mikopo yao kupitia benki ya CRDB mara baada ya kuzinduliwa kwa mpango huo baina ya taasisi hizo mbili leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mpango huo , Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw Adam Mayingu , alisema kuwa mpango huo wa kutoa mikopo kwa wanachama ulianza tangu Desemba 2014 kwa kupitia taasisi nyingine za kifedha.

Alisema kuwa PSPF na benki ya CRDB wamekubaliana kushirikiana katika kuendesha kwa pamoja huduma ya mikopo.Mikopo hiyo ni pamoja na mkopo wa elimu(education loan scheme), mkopo wa kuanzia maisha( startup life loan scheme) na mkopo wa viwanja(Nipo site na PSPF).

Alisema kuwa kwa upande wa mkopo wa elimu , mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yeyote ya elimu .Ngazi hiyo ni stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata mafunzo ya ufundi.

Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, alisema mwanachama aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa na mahitaji yake muhimu na kwa kutambua hilo, PSPF kwa kushirikiana na CRDB wameanzisha mpango huu ambapo mwanachama anaruhusiwa kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili awaeze kujipanga na maisha mapya ya ajira.

Kuhusu mkopo wa viwanja kwa wanachama, alisema kuwa huduma hii itawawezesha wanachama wa PSPF kukopa na kumiliki viwanja vya makazi ambavyo vinapataikana maeneo mbali mbali ya nchi.

“Lengo kubwa hapa ni kuwawezesha wanachama wa PSPF kumiliki viwanja vya makazi vilivyopimwa iii kuwaepusha dhdi ya ujenzi katika makazi holela, ambayo yamekuwa na gharama kubwa kuliko makazi yaliyopangiliwa”,alisema.

Alifafanua kuwa lengo kubwa la kuanzisha mikopo hiyo ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika masomo kupitia mkopo wa elimu , ndoto yake nyingine kupitia mkopo wa kuanzia maisha au mkopo wa viwanja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt. Charels Kimei, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ambapo CRDB sasa itawakopesha Wanachama wa PSPF kwenye maeneo ya elimu, viwanja na pesa za kuanzia maisha kwa watumishi wa serikali. Uzinduzi huo umefanyika Februari 27, 2017 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.
Dkt. Charles Kimei, akitoa hotuba yake kueleza jinsi benki yake ilivyofurahishwa na ushirikiano huo.
Bw. Mayingu akitoa hotuba yake kuelezea ushirikiano huo ambao lengo lake kubwa ni kupanuan wigo wa huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo.
Uzinduzi rasmi ukifanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...