MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imesaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na Kampuni ya SunShine Group kutoka China kwa miaka mitano kuanzia sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo wa makubaliano, Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Graceana Shirima alisema makubaliano hayo yataifanya TEA kuwa mratibu wa miradi ya kuboresha elimu hapa nchini huku Sunshine ikifadhili na kutekeleza miradi hiyo.
Kwa mujibu wa Shirima miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mara na Mtwara ambapo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule na vifaa itatekelezwa na kampuni hiyo huku akibainisha kwamba mikoa hiyo ndiyo yenye miradi mikubwa ya kampuni ya Sunshine.
“Miradi ya kwanza kutekelezwa kupitia makubaliano haya ni ujenzi wa maabara mbili za sayansi katika shule za sekondari Matundasi iliyopo Jijini Mbeya na miundombinu ya maji kwenye sekondari ya Bunda mkoani Mara ambapo Zaidi ya sh. Milioni 210 zitatumika,” alisema Shirima.
Akiishukuru TEA, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sunshine Goup, Tony Sun alisema kampuni yake inaona fahari kusaidia sekta ya elimu Tanzania huku akiahidi kuendelea kuwekeza katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Dk. Erasmus Kipesha akisaini mkataba wa makubaliano hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akisaini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, wa makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. Kushoto anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipanga, Dk. Erasmus Kipesha na Mwakili Mkazi wa Sunshin Group, Harison May.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...