Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini kabla ya Balozi huyo kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Idara hiyo ambao unalenga kuboresha zaidi huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto (upande wa pili) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.

Na Humphrey Shao, Globu ya jamii.

Idara ya uhamiaji imezindua mkataba wa huduma kwa wateja ambao utawawezesha kutoa hati ya kusafiria ndani ya siku tano bila kuchelewa.

Akizungumza na wahabari katika makao makuu ya idara ya uhamiaji jijini Dar es Salaam,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya amesema kuwa kama watumishi wa idara hiyo watashindwa kukidhi vigezo hivyo walivyojiwekea wananchi wana haki ya kulalamika na kutoa taarifa katika ngazi za juu.

“Tumejiwekea viwango kuwa wakati wote mtu kama ataomba pasipoti apewe ndani ya sikutano mkataba huo umeonyesha wajibu wa mtoaji huduma  kumuhudumia mteja vile inavyotakikana” amesema Balozi Yahya.

Ameongeza kuwa kuanzia sasa mteja ni mfalme pindi anapofika katika idara hiyo kuhitaji hati ya kusafiria na sasa ana fursa ya kulalamika pindi huduma atakayopata kuwa aitakuwa na radha.Amemaliza kusema kuwa kuwa kuanzia sasa watu wote watapewa huduma kwa heshima na taadhima kutoka idara ya uhamiaji.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Idara ya Uhamiaji. Mkataba huo ambao unalenga kuimarisha huduma mbalimbali za Idara hiyo pia umeelekeza kuanzia sasa Hati za Kusafiria (Pasipoti) zitatolewa kwa siku tano za kazi kwa watakaoomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akionesha machapisho ya mkataba wa huduma kwa wateja kati ya Idara ya Uhamiaji na wananchi.
Baadhi ya wananchi waliofika katika halfa ya uzinduzi wa mkataba huo.
. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa idara ya uhamiaji.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akisalimiana na watendaji wa uhamiaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...