Baaadhi ya watu mbalimbali wakitembelea banda la Tanzania, nchini Saudi Arabia, katika maonyesho ya utalii ya '(Travel and Tourism Pioneers Forum - 2017).
Maonyesho ya utalii nchini Saudi Arabia yaipaisha Tanzania
Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
Ubalozi
wa Tanzania nchini Saudi Arabia mwishoni mwa juma hili ulishiriki
katika maonyesho ya Safari na Utalii yajulikanayo kama '(Travel and
Tourism Pioneers Forum - 2017).
Maonyesho
ya TPF 2017 ambayo hufanyika kila mwaka kwa uandalizi Al Awsat Expo
chini ya uhisani wa Mwana Mfalme HRH Prince Dr. Seif al Islam bin Saud
bin Abdulaziz, yamefanyika kwa mafanikio huku ubalozi wa Tanzania
ukifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutangaza utalii wa Tanzania.
Akizungumza
katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E
Hemed Mgaza, alisema kwamba maonesho hayo yalikuwa maalumu kwa wafanya
maamuzi na viongozi wa asasi za utalii (decision makers and leaders and
tourisma leaders) nchini Saudi Arabia.
Balozi
wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, mwenye suti nyeusi
akizungumza jambo na wageni waliotembelea katika banda la Tanzania
kwenye maonyesho hayo.
Alisema kwamba kuwa banda la Tanzania lilifanikiwa kuonesha vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, hifadhi za taifa, maeneo ya kihistoria ya Zanzibar, kilwa na Bagamoyo.
Mazungumzo yakiendelea yakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia
Watu wakipata maneno juu ya utalii wa Tanzania nchini Saudi Arabia
Karibuni Tanzania.
“Tunashukuru
kwa kiasi kikubwa kushiriki katika maonyesho haya sambamba na Tanzania
kutangaza vivutio vya utalii wan chi yetu, tukiamini kuwa ni fursa
adhimu kwa nchi yetu.
“Tunaendelea
na juhudi za kutangaza nchi yetu ya Tanzania sambamba na kuwaonyesha
watu wa Saudi Arabia juu ya umuhimu wa kutembelea nchini kwetu ili
kujionea fursa mbalimbali za kiuchumi na utalii,” Alisema.
Kwa
mujibu wa Balozi Mgaza, miadi na majadiliano kuhusu kukuza utalii
(promotion of tourism) yalifanyika baina ya washiriki wa Tanzania na
mawakala wa utalii (tour operators) na wa usafiri (travel agents).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...