Na Karama Kenyunko, blog ya jamii
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), amewataka wananchi kuzibua mitaro ili kuepuka mafuriko yanayoweza kutokea katika mvua za masika za mwezi Machi hadi Mei Mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk. Agnes Kijazi amesema licha ya kwamba mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani na nyingeni juu ya wastani katika maeneo mingi nchini ni vema wananchi wakachukua tahadhari mapema.
Amesema kuwa, taadhari hizo zitasaidia wananchi kuondokana na kukumbwa na mafuriko kwa baadhi ya maeneo nchini, kuepuka vifo na magonjwa ya mlipuko.
Aidha amewataka wananchi kutunza maji katika mvua hizo zinazoanza kunyesha ili kuepuka athari za upungufu wa maji uliojitokeza
Aliongeza kuwa, msimu wa mvua za November hadi Aprili mwaka huu ni mahususi kwa maeneo ya Magharibi mwanchi, kanda ya kati, nyanda za juu kusini-magharibi, kusini mwa nchi na pwani ya kisini.
Amesema mvua katika mikoa ya Njombe, Songwe Ruvuma, Mtwara, Lindi, pamoja na eneo la Morogoro Kusini (Mahenge) zinatarajiwa kuwa za wastani.
Aidha aliongeza kuwa katika mvua zinazoendelea katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani na pia zinatarajiwa kuisha katika wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Aprili mwaka huu
"Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, kusini mqa Morogoro na ile ya kusini na pwani ya kusini inatarajiwa kuwa na mvua za wastani.
Dk Kijazi Aliongeza kuwa mvua za msimu huu zinatatarajia kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Ap. rili hadi wiki ya kwanza ya mwezi Mei mwaka hui.
Mkurugenzi wa Mkuu wa TMA Dk. Agnes Kijazi akizungumza na wanahabari juu ya mwelekeo wa mvua za masika za mwezi Machi hadi Mei mwaka huu.Leo jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakimsikiliza Dk. kijazi kwenye mkutano wa Uelekeo wa mvua za Masika mwezi Machi hadi Mei mwaka huu Leo jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa utafiti wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Ladislaus Chan'ga akifafanua jambo mbele ya wanahabari Leo jijini, kulia ni Mkurugenzi Mkuu Dk. Kijazi





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...