Na Karama Kinyunko-Glob ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeondoa kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk. Valentino Mokiwa.

Kesi hiyo imeondolewa leo baada ya Wakili ambaye ni muwakilishi wako kisha Askofu Mokiwa, Mathew Kabunga kuiomba Mahakama kuiondoa kwai hiyo chini ya kifungu cha sheria cha 23(2)(b).

Akiqasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba alisema" mheshimiwa, Nina hoja." " Baada ya kujadiliana na mteja wangu (Mokiwa) hayupo tayari kuendelea na kesi, tu naomba kuiondoa chini ya kifungu cha 23(2)(b).

Wakili wa upande wa wadaiwa, Emmanuel Nkoma amekubaliana na ombi hilo la mdai kwa kuwa yeye ndiye aliyepeleka shauri mahakamani.

Aidha aliiomba Mahakama wamuamuru mdai kulipa garama za kesi kwa kuwa wadaiwa walishaingia garama za kuwaweka mawakili na zile za kuendeshea kesi

Hakimu Simba hakuwa na pingamizi, aliwataka upande zote mbili kukaa na kujadiliana garama za kesi.Mapema Askofu Mokiwa alifungua kesi ya madai mahakamani akiiomba itengue uamuzi wa kuvuliwa uaskofu na kumtangaza kuwa askofu.

Dk. Mokiwa kwa kupitia kampuni ya uwakili ya M. B Kabunga and Co. Advocates, Mathew Kabunga, alifungua kesi hiyo namba 20, ya mwaka huu, dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Jacob Chimeledya na bodi ya wadhamini ya kanisa hilo, akipinga kuvuliwa uaskofu.

Kwa kupitia hati yake ya maadai, Dk. Mokiwa anadai kwamba waumini takriban 28, wa kanisa hilo, waliandika barua ikiwa na mashitaka 10, dhidi yake, lakini barua hiyo haikuwasilishwa kwake na ilionesha kuna nakala.

Januari 7, mwaka huu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Chimeledya alimvua uaskofu mkuu Dk. Mokiwa, kutokana na mashitaka 10, aliyofunguliwa na walei 32, wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, yakiwemo ya ufisadi wa mali za kanisa.
 Wakili Mathew Kabunga,  anayemuwakilisha Askofu Valentino Mokiwa, akiondoka katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya ombi lake la kuiondoa kesi ya madai iliyofunguliwa na Askofu Mokiwa kupinga kuvuliwa uaskofu kuondolewa.
Wakili  wa wadaiwa katika kesi ya madai iliyofunguliwa na Askofu Mokiwa,  dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglicana Tanzania, Jacob Chimeledya na Bodi ya wadhamini ya kanisa hilo, Emmanuel Nkoma akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...