Baadhi ya wapiga picha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Rubani wa parachuti, David Eris kutoka kampuni ya HOT AIR Safaries, mara baada ya ziara ya kuitembelea Hifadhi ya Maasai Mara, nchini Kenya. Wapiga picha hao walitembelea hifadhi hiyo kufuatia mualiko kwa kampuni ya kutengeneza kamera aina ya Canon ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kamera mpya aina ya Canon D5 Mark IV, ambapo wapiga picha hao waliweza kupatiwa uzowefu wa kamera hiyo mpya iliyoongezewa ubora katika upigaji picha na video pia. Mpiga picha na Blogger, Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog (wa kwanza kulia waliopiga goti) ndiye aliyekuwa mwakilishi wa wapiga picha kutoka Tanzania. na zifuatazo ni baadhi tu ya picha alizopiga katika ziara hiyo.
Twiga
Duma wa Maasai Mara wakiwa mawindoni
Mfalme wa Pori, Simba akiwa kala pozi.
Swala na Twiga.

Pundamilia akilia.
Simba jike akipanga mbinu za kwenda kuwinda wakati Dume akisubiri.
Nyati wa Maasai Mara.
Muonekano wa vivuli vya baadi ya wapiga picha hao wakakati wa kuchomoza kwa jua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...