Askari wawili wanaodaiwa kuiba mafuta ya ndege ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na raia wengine wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kujibu tuhuma za kula njama na kuhujumu nchi.

Mwendesha Mashtaka wakili wa serikali mwandamizi Nassoro Katuga akisaidiana na wakili Leornad Chalo waliwataja askari hao kuwa ni F. 8419 Koplo Bahati Nyerema Msilimani (33), mkazi wa Ukonga Kota za Airwing na F.9901 PC Benaus (34), anayeishi Ukonga Madafu.

Wengine ni  Iddy Juma Nyangas (42), mlinzi wa Moko mkazi wa Vingunguti kwa Mnyamani na Ramadhani Bakari Mwinshehe (52), fundi wa ndege mkazi wa Yombo Buza.

Mbele ya Hakimu Voctoria Nongwa imedaiwa kuwa, kati ya Machi 1 hadi 17 mwaka huu, katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la kuhujumu.

Iliendelea kudaiwa kuwa, siku na mahali hapo washtakiwa hao kwa ajali ya kuhujumu manufaa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, bila kuwa na uhalali kisheria walitoboa ndege kukinga lita 280.6 kutoka kwenye ndege ya ATCL namba 5-HMWF-DASH 8 Q 300.

Iliendelea kudaiwa kuwa kitendo hicho kilikuwa ni kuingilia utoaji wa huduma maalumu kwa jamii ya ndege.
Watuhumiwa wa Uhujumu uchumi wa mafuta ya ndege ya serikali (ATCL) wakiwa kizimbani.

Hata hivyo, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mashtaka yao yako chini ya sheria ya uhujumu uchumi na DPP hajatoa kibali cha kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu Kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo, Mahakama imewaachia washtakiwa hao kwa dhamana kwa vila hakuna kibali cha DPP  kinachopinga dhamana na pia mahakama ya kisutu inayomamlaka ya kutoa dhamana kwa kesi isiyozidi shilingi milioni kumi na katika mashtaka yanayowakabili washtakiwa haionyeshi garama za mafuta washtakiwa wanazodaiwa kuhujumu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 27,mwaka huu,.

Wakili Katuga ameiarifu mahakama kuwa, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa wako nje kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja walioweka dhamana ya shilingi milioni moja.

Aidha mahakama imewataka washtakiwa kutosogelea maeneo yao ya kazi na vilevile kutyosafiri nje ya Dar esSalaam bila kibai cha mahakama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...