Globu ya Jamii inatoa taarifa kwa wenye ndugu, jamaa na marafiki  waliosafiri kwenye mabasi ya abiria ya Abood na Happy Nation kutoka Mbeya kwenda jijini Dar es salaam kwamba yamepata ajali mlima Kitonga leo mchana. Taarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wameeleza kuwa katika ajali hiyo wamejeruhiwa abiria 12.

Mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo alieleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi la Abood kukosa breki na kuligonga roli la FM ambalo halikuanguka ila liligonga Fuso iliyokuwa imebeba ndizi na kutumbukia korongoni baadae likaigonga basi la Happy Nation na mabasi yote kutumbukia korongoni .
 
Taarifa rasmi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Iringa Kamanda wa Jeshi la zimamoto mkoa wa Iringa Kenedy Komba akiwa eneo la tukio ametihibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akielezea kuwa  taarifa za awali majeruhi ni 12 na kati ya hao majeruhi watatu wamekimbizwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi, na kwamba hakuna vifo vilivyotokea katika ajali hiyo.
 
Moja ya Lori lililogongwa na kumbukia korongoni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...