Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MBUNGE wa jimbo la Mji wa Kibaha,mkoani Pwani Mhe. Silvestry Koka,awataka vijana kuacha kujibweteka na kuwa tegemezi,badala yake wajikite katika shughuli ndogondogo ili kujiinua kiuchumi. Amesema anatambua tatizo kubwa ni kukosa mitaji kwa vijana lakini,nguzo pekee ya kupata msaada kirahisi ni kuunda vikundi ili kuweza kuwawezesha mikopo na masuala mengine ya maendeleo.
Mhe. Koka aliyasema hayo mjini Kibaha baada ya kuzindua mradi wa chama cha madereva wa pikipiki ,Mailmoja wa mashine ya kuoshea magari.
Aliwaomba wale walioanza ujasiliamali kuacha ubinafsi bali wawasaidie wengine wasiojua ili hali waweze kutoka kimaisha pasipo kukaa vijiweni bila kuwa na mwelekeo wowote.Aidha Koka aliwasihi madereva hao kujenga umoja na mshikamano utakaowasaidia kulinda maslahi na faida wanazozipata.
Aliahidi kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana na makundi mengine ikiwemo wanawake ili kuweza kupiga hatua kiuchumi jimboni humo.
Mbunge huyo,alifafanua kwamba tangu aanze uongozi wake ameshasaidia makundi mbalimbali ya ujasiliamali ya wanawake na vijana zaidi ya sh.mil.180 kutoka mfukoni mwake.“Nimejipanga kuendelea kuviwezesha vikundi hivyo kwani ni moja ya kutimiza vipaombele vyangu nilivyojiwekea japo kuwa vijana bado hawajajipanga kikamilifu”alieleza Koka.
Awali,Koka alizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa kata ya Mailmoja na anaendelea na ziara yake aliyoianza jimboni hapo.
Mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha Mhe. Silvestry Koka akizindua mradi wa kuosha magari wa chama cha madereva pikipiki Mailimoja Kibaha.
(Picha zote na Mwamvua Mwinyi)
(Picha zote na Mwamvua Mwinyi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...