Na Saleh Jabir
Baadhi ya watu nchini kwetu Tanzania na nchi za jirani, wamekuwa wakichanganya maana ya neno utandawazi na neno mtandao. Baadhi yao, ambao waliosikika huwa wanazungumzia jambo lenye mantiki ya utandawazi lakini wakitumia jina la mtandao. 
Ningependa kuchukua fursa hii kutoa mchango wangu kwenye mada ya ‘utandawazi’ na iwe kama ni mchango wangu kwa taifa na kwa Watanzania wenzangu kwa ujumla.

Kabla ya kuanza kuelezea maana ya utandawazi, ningependa kujitambulisha kuwa mimi siyo mwanaharakati, bali mimi ni mzalendo wa nchi yangu na naamini kuwa mchango wangu wowote mdogo ninaoutoa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yangu utaleta mabadiliko kwa kiasi fulani kwa kutumia makala zangu kwa faida ya jamii au kwa taifa kama siyo dunia kwa ujumla. Lakini lengo langu katika makala hii ni kuangaza nchini kwetu Tanzania tu na kutolea mfano baadhi ya mataifa mengine ambayo ni rafiki na Tanzania juu ya suala la uchumi wa utandawazi.
Utandawazi (Globalisation) ni nini? Utandawazi ni hali ya muingiliano wa kifikra au kimatendo baina ya nchi moja na nchi nyingine, au baina ya mtu mmoja na mtu mwingine ambao wapo nchi tofauti. Kawaida muingiliano huu, unakuwa ni muingiliano wa kiuchumi au kisiasa au kiutamaduni, na katika muingiliano huu, si lazima nchi moja ifaidike zaidi ya nchi nyingine.
Sasa tujiulize, je, nadharia hii ni mbaya? Jibu ni ndiyo na hapana! Kwasababu utandawazi una faida zake na una hasara zake kwa taifa huru kama taifa letu la Tanzania, lakini mara nyingi ukiangalia hasara zake ni kubwa na zinapotoweka zinakuwa ni hasara zisizoweza kurejeleka, iwapo utandawazi utatanda kwa miaka mingi katika taifa na hususan ukitanda kwenye kila ngazi ya taifa.
Baadhi ya sababu hizo nilizielezea juu juu katika makala yangu (2013) niliyogusia utandawazi, lakini sikuuelezea kwa kina sana (2013, Nini kinachofuata baada ya katiba mpya?).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...