IDADI
ndogo ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki kunachangia pakubwa kuchakaa
haraka kwa fedha.
Hayo
yamesemwa na Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma
za Kibenki, Bw.Abdul M.Dollah, wakati akijibu maswali ya Washiriki wa Warsha ya
Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, inayoendelea kwenye ukumbi wa BoT tawi la
Zanzibar, leo Machi 30, 2017 waliotaka kujua ni kwa nini fedha za noi
zinachakaa haraka hususan shilingi 500 na shilingi 1,000/_
“Ubora
wa karatasi zinazotumika kutengenezea noti zetu unalingana, lakini matumizi
makubwa ya noti hizo zilizotajwa, zinapita kwenye mikono ya idadi kubwa ya watu
na hivyo kupelekea kuchoka haraka.” Alifafanua
Akifafanua
zaidi alisema, Idadi ya Watanzania kwa sense iliyofanyika mwaka 2012 ni Milioni
48, lakini kati ya hao ni Watanzania Milioni 4 tu ndio wanatumia huduma za
kibenki, (kuwa na akaunti benki), na idadi ya waliosalia, hutunza wenyewe fedha
hizo.
Utunzaji
mbaya wa fedha na hali ya hewa ya baadhi ya maeneo nchini, huchangia kuchakaa
haraka kwa fedha “ Kwa mfano, kule Tanga maeneo ya Lushoto na Kibondo mkoani
Kigoma, kutokana na rangi ya udongo wa sehemu hizo, utakuta fedha inachakaa
haraka sana, alisema Bw.Dollah.
Akielezea
majukumu ya Kurugenzi ya Huduma
za Kibenki ya Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Dollah alisema, Sheria namba
Nne (4) ya BoT, imeipa kurugenzi hii jukumu la kusanifu, kutoa, kusambaza na
kuharibu fedha,(noti na sarafu), zilizochakaa.
Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M. Dollah, akitoa mada juu ya Huduma za Kibenki Benki Kuu ya Tanzania.NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Washiriki wa semina, wakiangalia noti ya Sh. 10,000, ili kutambua kama ni halali au so halali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...