Shirika la Datang Telecom International Technology Company Limited la Serikali ya China lina mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza vifaa vya mawasiliano nchini kwa ushirikiano na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Rais wa Shirika hilo Yuan Yong ametoa kauli hiyo 1-Mar-2017 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.

Yuan Yong amemweleza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Serikali ya China pia ina mpango wa kuikopesha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kiasi cha shilingi bilioni 600 ili kuipa uwezo wa kiteknolojia na kupanua mtandao wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini hasa vijijini.

Rais huyo amesema lengo la mkakati huo ni kuifanya TTCL kuwa Kampuni bora inayotoa huduma za mawasiliano kwa njia ya kisasa kuliko kampuni yeyote katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan  akizungumza na Rais wa Shirika la Datang Telecom International Technology Company Limited la Serikali ya China Bw.Yuan Yong (kulia) pamoja na ujumbe wake, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
10:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Shirika la Datang Telecom International Technology Company Limited la Serikali ya China Bw.Yuan Yong na ujumbe wake mara baada ya kupokea taarifa ya mpango wa serikali ya China wa kuikopesha TTCL ili kuipa uwezo wa kiteknolojia  na kupanua mtandao wa mawasiliano vijijini na mijini pamoja na kujenga kiwanda cha kutengeneza vifaa vya mawasiliano hapa Tanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...