MSHAMBULIAJI wa Yanga wa kimataifa kutoka nchini Mzimbabwe Donald Ngoma amesema ataondoka katika klabu hiyo kukwepa mambo ya ovyo ya uongozi.

Ngoma amesema hayo wakati akizungumzia tuhuma dhidi yake juu ya kutocheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba Jumamosi, Yanga ikichapwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Amesema kwamba ataondoka Yanga baada ya kuchoshwa na 'madudu' ya uongozi wa timu, mchezaji huyo amesema kwamba mashabiki na wapenzi wa Yanga wamekuwa wakimshutumu na kumtukana kutokana na taarifa zisizo za kweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu yeye. 
  
“Nimekuwa kimya wakati wote nikitukanwa juu ya sababu za kutocheza, wakati ukweli ni kwamba mimi nina maumivu ya goti. Taarifa nyingi zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba sitaki kucheza kwa sababu ninataka kuondoka katika timu, nashangaa wapi wanapata hizo taarifa,”amesema Ngoma.

Amesema Daktari ambaye Yanga walimtumia kumtibu yeye alikuwa ‘tapeli’ na ameilia fedha klabu bila kufanya kazi yoyote. “Daktari alikula fedha za viongozi wa klabu na kuwadanganya kwamba alikuwa ananitibu amenipeleka hospitali, wakati ukweli ni kwamba nilikuwa ninatibiwa katika hospitali nyingine kwa gharama zangu mwenyewe,”amesema Ngoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...