
Akizungumza na waandishi
wa habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amesema kufuatia tuhuma
mbalimbali za uendeshaji, zinazolikabili Shirika hilo ambazo zimekuwa
zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa.
Simbachawene amesema Mnamo
Machi, 4 mwaka huu Rais Magufuli ametengua rasmi nafasi ya Mtendaji huyo ili kupisha
uchunguzi wa tuhuma hizo.
Amefafanua kuwa kumekuwepo malalamiko dhidi ya Mtendaji Mkuu wa
wa shirika la Elimu Kibaha ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI iliunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi dhidi ya malalamiko
hayo na kugundua kuwepo kwa changamoto
katika uendeshaji wa Shirika hilo.
“Ni kweli tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika
la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na Shirika hilo
zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka kukurupuka kufanya
maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi na matokeo ya
uchunguzi huo yanapelekea kuwepo kwa hoja
zinazohitaji uchunguzi zaidi,” ameeleza Waziri Simbachawene.
Ameongeza kuwa ili
uchunguzi huo uweze kufanyika kwa uhuru Mhe. Rais ameamua kumsimamisha kazi
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi
yake.
Waziri amesema uamuzi wa
kumsimamisha umechukuliwa kwa kuwa tuhuma na malalamiko mengi ya awali yaliyojitokeza dhidi yake yanajenga hoja ya kuhitajika
kufanyika kwa uchunguzi zaidi ambapo kwa sasa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa
Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...