Na Zainab Nyammka, Globu ya Jamii
Msafara wa mabingwa wa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC , umewasili salama jijini Dar es salaam ukitokea Morogoro walipokwenda kucheza na Mtibwa Sugar kwa matokeo ya sare ya 0- 0.
Msafara huo umeelekea moja kwa moja kambini kwa maandalizi ya michezo miwili muhimu itakayofanyika kesho machi 7, 2017 dhidi ya Kiluvya United uwanja wa Taifa na machi 11, klabu bingwa Afrika dhidi ya Zanaco FC.
Timu imeendelea na mazoezi jioni ya leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kesho robo fainali kombe la FA dhidi Kiluvya ya kutoka mkoani Pwani .
Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamiana amesema kuwa licha ya ratiba ngumu kuikabili timu yake lakini amesema yupo tayari kupambana na vijana wake ili kuhakikisha klabu inapata matokeo mazuri katika michezo yote miwili.
Wapenzi , wanachama , mashabiki na wadau wa soka mnaombwa kujitokeza kwa wingi katika michezo yote miwili ili kuipa sapoti timu hiyo .
Mbali na hilo, droo ya kombe la Shirikisho hatua ya saba au robo fainali inatarajiwa kufanyika kesho baada ya kupatikana kwa mshindi wa mechi kati ya Yanga na Kiluvya na kuungana na timu za Simba na Azam FC za Dar es Salaam, Mbao FC ya Mwanza, Tanzania Prisons ya Mbeya, Madini ya Arusha, Kagera Sugar ya Bukoba na Ndanda FC ya Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...