Kwa mara nyingine tena redio EFM imetoa pikipiki 2 katika wilaya mpya ya Kigamboni kupitia shindano lake la shika ndinga ambalo hufanyika kila mwaka ikiwa ni moja kati ya njia ya kuwawezesha kiuchumi wasikilizaji wa redio hiyo na pia kuendelea kuwa nao karibu zaidi.
Shindano hilo Linahusisha michezo mbalimbali ukiwemo wa kushika gari ambapo washindi mbalimbali hufanikiwa kujishindia pikipiki kila wailaya na washindi wawili katika fainali hufanikiwa kuondoka na gari aina Kirikuu(SUZUKI CARRY). Mwaka huu shindano hilo limefanyika kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi ya tarehe 25/03/2017katika viwanja vya Machava wilaya ya Kigamboni
Shindano hilo limeboreshwa kwa kiasi kikubwa mwaka huu kwa kuwa litaacha pikipiki aina ya San moto 12 kutoka kampuni ya MOSAN company limited katika wilaya 6 ambapo kwa mkoa wa Dar es salaam wilaya hizo ni Kigamboni, Temeke, Ilala, Kinondoni na kwa mkoa wa Pwani ni Kibaha na Bagamoyo.
Majaji wa shindano la shika ndinga wakijadili mbinu na mikakati ya shindano hilo.
Washehereshaji wa tamasha hilo ni Adam Melele Swebe Santana(kulia) na Denis Rupia (Chogo)
Washiriki wakike waliofuzu kuingia katika kumi bora wakichuana kwa kushika ndinga ambayo ni hatua ya mwisho ya mashindano.
Baadhi ya washiriki wakiume wakichuana katika hatua ya kwanza ya shindano inayohusisha mchezo wa mbio za magunia ili kufuzu kuingia katika mchezo wa pili.
Baadhi ya washiriki wakike wakichuana katika hatua ya pili ya shindano inayohusisha mchezo wa kujaza maji kwenye vikombe kutoka hatua moja kwenda nyingine ili kufuzu kuingia katika kumi bora na kufanikiwa kuingia hatua ya mwisho ya kushika ndinga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...