Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing hii leo hii tarehe 28/3/2017 akiwa ofisini kwake amefanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Shaidi Mchembe.Katika mazungumzo yao ambayo yalijikita katika maeneo makubwa matatu, ambayo ni Kilimo cha Kibiashara kwa ushirikiano na Serikali ya China, Kupatia vikundi vya wanawake viwanda vidogo vidogo vya kukamua mafuta ya alizeti, pamoja na kuweka  Mkakati wa kujenga Soko la Kisasa la Mahindi na ghala la kuhifadhi chakula.


Mhe Mchembe amemwambia Balozi huyo kwamba kutokana na ukweli kuwa mvua zinazoendelea nchini zimeliweka Taifa katika mazingira mazuri ya kuvuna chakula kingi, ni vizuri pia kujipanga ili ziada iuzwe vizuri bila kumnyonya mkulima kama ilivyokuwa kwenye zao la korosho.
"Kauli ya Mhe. Rais Magufuli ya hapa kazi tu, ilimfanya kila mtu akafanye kazi hivyo kilimo kimefanyika cha kufa na kupona. Tunamshukuru Mungu kwa hali ya hewa nzuri, alisema Mhe Mchembe.

Katika mazungumzo hayo Balozi Youqing alisema Serikali ya China itaendelea kutoa misaada na kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa katika sekta ya Viwanda, Kilimo na Mifugo Endelevu kama ambayo alimuahidi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Steven Kebwe.

Aidha alimuahidi kutembelea Mkoa wa Morogoro mapema mwezi wa nne 2017 ili kitimiza ahadi yake.Mkuu wa Wilaya alimshukuru Balozi Youqing kwa kupeleka Wakuu wa Wilaya 20 nchini China kwa mafunzo ya Serikali za Mitaa ambapo nae alikuwa miongoni mwao.Vile vile Mkuu wa Wilaya huyo alimkaribisha Balozi Youqing Wilayani Gairo ili kujionea mafanikio ya mafunzo hayo.

 Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing akimkaribisha kabla ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Shaidi Mchembe ofisini kwake jijini Dar es salaam leo
 Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Shaidi Mchembe ofisini kwake jijini Dar es salaam leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...