Mshambuliaji Mbwana Samatta akichuana na beki wa Botswana kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika mwishoni mwa wiki na Tanzania kufanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-0.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta ameondoka kurejea Ubelgiji na hatakuwepo kwenye kikosi kitakachomenyana na Burundi leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Samatta aliyefunga mabao yote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana Jumamosi, amelazimika kurejea ili kuwahi maandalizi ya klabu yake kwa mchezo wa Robo Fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Celta de Vigo nchini Hispania Aprili 13. 

Mbwana Samatta atakosekana leo kwenye mchezo dhidi ya Burundi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Kwa kumkosa Samatta, kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amemuanzisha Ibrahim Hajib kama mshambuliaji kiongozi akicheza na kiungo Farid Mussa, huku pembeni akiwatumia kiungo Muzamil Yassin kulia na winga Simon Msuva kushoto.

Kwa ujumla kikosi cha Stars leo kipo hivi;

 Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Salim Mbonde, Himid Mao, Muzamil Yassin, Salum Abubakr ‘Sure Boy’, Ibrahim Hajib, Farid Mussa na Simon Msuva.

Katika benchi watakuwapo 

Said Mohammed, Hassan Kessy, Gareiel Michael, Hassan Kabunda, Jonas Mkude, Mbarak Yussuf, Abdulrahman Juma, Shiza Kichuya na Frank Domayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...