Na Benny Mwaipaja, WFM-Morogoro

Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango nchini wametakiwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuiletea nchi Maendeleo ya haraka kupitia falsafa ya uchumi wa viwanda utakao iwezesha nchi kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kusimamia matumizi yake ipasavyo.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, wakati akifungua mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika mjini Morogoro kwa siku mbili.

Bi. Mwanyika amesema kuwa Mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi, yana malengo ya kuongeza tija, ufanisi na ushirikishwaji wa wafanyakazi katika uongozi wa pamoja mahali pa kazi kama agizo la Rais Na. 1 la mwaka 1970 likisomwa pamoja na miongozo mingine linavyo elekeza. 

Aidha amewataka wajumbe wa Baraza hilo kukumbuka maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kuhusu kusimamia ukusanyaji wa mapato na nidhamu ya matumizi ya Fedha za Umma, ili kujenga uchumi wa Viwanda na kufikia maendeleo stahiki.

“Tuunge mkono juhudi za Serikali kwa kutafsri maelekezo ya viongozi kwa vitendo ili kuthibitisha msemo usemao Wizara ya Fedha na Mipango ndiyo moyo wa Serikali” alisisitiza Bi. Mwanyika.
Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa, akitoa nen0 la shukrani baada ya hotuba iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, akifungua mkutano wa Baraza hilo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mjini Morogoro.
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa makini maelezo ya mafanikio ya Mkutano wa Baraza hilo kwa mwaka 2015/2016 ambayo ni pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi, Mkutano uliofanyika Mjini Morogoro.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Cyprian Kuyava, akizungumza wakati wa Mkutano wa 13 wa Baraza hilo, Mjini Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...