Wito umetolewa kwa wananchi ambao wanafanya shughuli za uvuvi Mkoani Geita,kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuwafichua wale ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli ya uvuvi haramu katika mialo iliyopo Mkoani Humo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga wakati wa zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi kwenye Mwalo wa daladala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo zilizokusanywa ndani ya miezi miwili kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu.

Aidha mh Kyunga amesema kuwa uhifadhi wa rasilimali zilizopo kwenye ziwa viktoria ni muhimu kwa kila mwananchi kwani endapo
uvuvi haramu ukiachiwa madhara yake yanaweza kuwa ni makubwa kwa viumbe ambavyo vipo katika ziwa.

“Ndugu wananchi kwa kweli uhifadhi rasilimali zilizomo katika ziwa letu hili ni muhimu ,ni muhimu kwa sasa na vile vile kwa baadae isipokuwa mimi nisisitize sisi wote hapa kwa ajili ya ustawi wetu na vizazi vijavyo tuone kwamba tuna wajibu wa kuhifadhi mazingira na matumizi bora ya ziwa letu hili,tukilivuruga kama hawa wenzetu wanavyolifuruga kwa kuendesha uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira hasara ambayo wanatuachini ni kubwa sana hawa watu kwa lugha nyingine naweza kusema ni wachawi”Alisema Kyunga
Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiteketeza
dhana haramu ambazo zimekamatwa katika oparation iliyofanyika kwenye
mialo iliyopo Mkoani Geita lengo likiwa ni kutokomeza uvuvi haramu ambao
umeendelea kwa kasi kwenye mialo ya Izumacheli na Mganza.
Baadhi ya wananchi wakivuta kokolo wakipeleka eneo la kuchomea.
Dhana haramu za uvuvi zikiwa zimekusanywa kwaajili ya kuchomwa kwenye mwalo wa dala dala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo.
Meza kuu ikongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,wakisiliza kwa makini
taarifa ambayo ilikuwa ikisomwa na afisa uvuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...