Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi ameagiza Kliniki tembezi ya huduma za kibingwa kwa mkoa wa Singida kuwa endelevu huku akizielekeza halmashauri kuandaa mpango wa utekelezaji wa zoezi hilo kwakuwa linagusa maisha ya wananchi wa hali ya chini.

Dokta Nchimbi ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Iambi Wilayani Mkalama ambako zoezi la kliniki tembezi ya madaktari bingwa wa fani nane kwa Mkoa wa Singida lilikuwa linahitimishwa.

Amesema mara baada ya kukamilika kwa halmshauri zote saba mpango wa kuanza kutoa huduma za kibingwa kwa awamu ya pili uanze mara moja kwakuwa wagonjwa wengi walionufaika ni wale webnye kipato duni na walikuwa wameshakata tama ya kupata matibabu.

Dokta Nchimbi ametembelea wodi ya wanawake waliofanyiwa upasuaji na daktari bingwa wa wanawake, wodi ya akina baba waliofanyiwa upasuaji wa magonjwa ya tezi dume na matatizo ya njia ya mkopo pamoja, ametembelea chumba cha upasuaji wagonjwa wa macho na kumalizia wodi ya watoto waliofanyiwa upasuaji kutokana na matatizo ya mfumo wa upumuaji na midomo sungura.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akitoa mchango wa fedha kwa ajili ya upasuaji wa macho kwa mgonjwa aliyekosa fedha kiasi cha shilingi elfu thelathini kwa ajili ya huduma za kibingwa Wilayani Mkalama.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata hududma za kibingwa katika hospitali ya Iambi ya Wilayani Mkalama.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipanda Mkorosho katika shamba la Mkulima wa kijiji cha Gumanga wilayani Mkalama kama hamasa kwa wananchi wengine wapande zao hilo.
Wananchi wa kijiji cha Nkungi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakisaidiana kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima ili kuhamasisha kilimo hicho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...