Katika
kuisaidia benki ya damu hapa nchini, wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar
wamejitokeza kwa wingi na kujitolea kuchangia damu katika kuendeleza
mwitikio huo kwa jamii ulioanzishwa na Kampuni hiyo wiki iliyopiata
katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam.
Zoezi hili ambalo linaratibiwa na Kitengo cha uwajibikaji kwa jamii (CSR) cha Kampuni hiyo, limelenga kusambaza upendo kupitia shughuli hii ya uchangiaji damu ili kuiwezesha benki ya damu sambamba na kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu.
Shughuli hiyo ya uchangiaji iliyofanyika katika makao makuu ya Ofisi za Zantel-Zanzibar, ilishuhudia mwitikio mkubwa kutokana na wingi wa wafanyakazi wa Zantel kujitokeza, pamoja na baadhi ya wananchi wakishiriki kuchangia damu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la uchangiaji damu, Mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Musa Baucha aliwashukuru watu wote walioshiriki na kutoa rai kwa makampuni mbalimbali pamoja na wananchi kuwa tayari kujitolea kwenye shughuli kama hizo wanapotakiwa kufanya hivyo.
“Tunayo furaha kwa mwitikio huu wa kukubali kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu kwa kuonyesha upendo hususan wafanyakazi wa Zantel Zanzibar. Niwaombe muendelee na moyo huu huu wa kujitolea pindi mnapohitajika kushiriki kwenye shughuli nyingine kama hizi,”alisema.
Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kampuni ya Zantel-Zanzibar Mohamed Musa Baucha akijiandaa kuchangia damu wakati wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lilloandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar Gabriel Laurent.
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Mohammed Ali akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
Afisa mdhibiti wa Rasilimali watu wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Said Habibu akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...