Uongozi wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zanzibar (ZFU) unafikiria kuandaa mpango maalum wa kuwawekea Bima ya Afya wanachama wake kwa lengo la kuwakomboa wakati wanapokumbwa na matatizo ya Kiafya.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chama hicho Mohamed Abdulla Laki  akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa ZFU wakati wa mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Mohamed Abdulla Laki alisema inakuwa aibu na masikitiko makubwa  pale  Msanii ambaye ni kioo cha jamii anapoonekana akidhalilika wakati akitafuta huduma za matibabu kipindi anaposumbuiliwa na matatizo ya kiafya bila ya kupata msaada wa uhakika.

Alisema wapo baadhi ya wasanii katika zama tofauti zilizopita waliowahi kukumbwa na kadhia hiyo na kuishia katika mazingira ya kusikitisha huku jamii ikijisahau kwamba  wasanii hao walitumia nguvu, ujuzi na uzalendo wao katika kuielimisha jamii hiyo kupitia fani ya sanaa.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Uongozi huo ulifika kumtaarifu rasmi azma yao ya kuandaa Tamasha la kuibua vipaji vya wasanii wanchanga Zanzibar linalotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu.


Balozi Seif  akiwa katika picya ya pamoja na Uongozi wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya  aliofanya nao mazungumzo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Msanii Jamila Abdulrahman { Babyjay } na Mohamed Abdulla Laki. Kushoto  ya Balozi Seif  ni Msanii Abdulkheir Chum na Msanii Rashid Mustapha ambae ni msemaji wa Chama hicho. Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...