Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar , Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji hufanyika hapo ambapo ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jeraha la mmoja wa wananchi wa eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi, ambaye wiki chache zilizopita alijeruhiwa na mapanga na watu wanaofanya matendo ya uhalifu katika eneo hilo.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma, akizungumza na vyombo vya habari juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya uhalifu katikaeneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo, wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) kutembelea maeneo sugu ya uhalifu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...