Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka vijana kutumia muda wao kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu badala ya kupoteza muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii kwakuwa kusoma vitabu ndiyo msingi mzuri wa elimu.

Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua Kitabu cha “Colour of Life” kilichoandikwa na Mwandishi Bi. Ritha Tarimo ambapo katika hotuba yake aliyoitoa mbele ya wageni waalikwa amesisitiza suala la vijana kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili kukuza elimu yao.

Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa, baadhi ya vijana siku hizi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii badala ya kujisomea, hivyo amewashauri wajifunze kutoka kwa Mwandishi wa Kitabu hicho ili waje kuwa waandishi hodari wa kutegemewa na Taifa.

Sambamba na rai hiyo, Waziri Mwakyembe amempongeza Bi. Ritha Tarimo kwa juhudi zake kubwa na maarifa katika kutunga na kuandika kitabu hicho ambacho amesema kuwa kitabu hicho ni kizuri na kina maudhui mazuri kwa vijana hususani wanafunzi, hivyo ameitaka jamii kumuunga mkono kwa kukisoma ili jamii ipate kuelimika.

“Ukimkuta mtu kama Ritha Tarimo anaandika kitabu katika kipindi hiki ambapo vitabu vinaonekana kuondolewa kwasababu ya maendeleo ya teknolojia, ni vema kumpa moyo na kumuunga mkono kwakuwa yeye ametuonyesha Watanzania kuwa hata sisi tunaweza, na kitabu hiki niwaambie ukweli kina maudhui ya kumtia moyo kijana ya kutokata tamaa katika maisha”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo. 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. 



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha "Colour of Life"leo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo pamja na wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA/HABARI NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mh Mwakyembe, vijana na watu wa rika zote wanaweza wasikuelewe kuhusiana na usomaji wa vitabu, si kwa sababu wamelelewa katika mazingira ya kuwa adui wa vitabu (tangu mashueni) laa hasha bali ni kwasababu wengi wetu tunakuwa 'driven' na habari za kimbea na kusengenyana ambazo hatutazipata kwenye ivyo vitabu. Tanzania tunakazi kubwa ya kuwaelimisha sio tu watoto na vijana bali pia wazazi wote kuhusu umuhimu wa kusoma vitabu. Ni jambo kawaida kwa mtanzania mwenye elimu ya shahada ya uzamili kufariki bila kuwahi kusoma kitabu hata kimoja (nje ya utaratibu wa shule)kwa ajili ya kujiongezea maarifa. sasa kama uyu mtanzania mwenye elimu ya shahada ya uzamili yuko ivyo, vipi kuhusu hao wenye elimu za chini kuliko yeye? Apo ndipo tone ukubwa wa tatizo la usomaji wa vitabu. Tubadilike!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...