Na Ofisa Habari Mufindi 
 Serikali Wilayani Mufindi Imewataka wajumbe wa kamati za Shule na viongozi wa Serikali za vijiji kwa kushirikiana na wazazi, kutekeleza mpango wa utoaji chakula cha mchana kwa wanafunzi wanapokua shuleni kwa lengo la kuongeza ufanisi wakati wa kujifunza na kuleta matokeo chanya. 
 Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi iliyofanyika Kata ya Nyololo Wilayani humo. 
 Mkuu huyo wa Wilaya amesema, mpango wa utoaji wa chakula Shuleni ambao wazazi hutakiwa kuchangia kwa mujibu wa sera ya Elimu pasipo malipo, husaidia kuleta usawa kati ya walionacho na wasionacho, kuimarisha mahudhurio na kutunza muda wa ratiba za shule na kusisitiza kuwa endapo mambo haya yote yatafanyika kiusahihi yanamchango mkubwa wakati wa ujifunzaji ulio bora kwa wanafunzi darasani. 
 Maadhimisho ya siku ya kusoma katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi yanalengo la kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji wa stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) huku yakiambatana na maonyesho ya Elimu na utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye kuandika, kusoma na kuhesabu. 
 Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imekua miongoni mwa Halmashauri ambazo shule zake zinafanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kwani mapema mwaka jana Halmashauri ya Mufindi ilishika nafasi ya sita  kwenye mitihani ya darasani la nne  kati ya Halmashauri 185.
Pia mwaka 2014 iliweka rekodi ya kukumbukwa ambapo shule yake ya kata ya Igowele iliongoza kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa kidato cha sita
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi iliyofanyika Kata ya Nyololo Wilayani humo.


Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akimvisha zawadi ya Begi la shule mmoja kat ya Wanafunzi wa darasa la kwanza  waliofanya vizuri kwenye stadi za kuandika ,kusoma na kuhesabu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...