Kituo cha utangazaji cha EFM redio kimecheza mechi ya kirafiki baina yao na madereva daladala siku ya leo ya tarehe 24/05/2017 katika Kiwanja cha Tanganyika Packers kuanzia saa kumi Jioni, ambapo watangazaji wa Redio hiyo wamechuana vilivyo na wadau wao wakubwa.
Redio hii ya vijana na jamii kwa ujumla imezidi kutoa kipaumbele kwenye michezo hususani mpira wa miguu kwani imekua ikicheza mechi nyingi za kirafiki kila inapobidi ili kuhakikisha inajenga mahusiano mazuri na jamii inayoizunguka kama wadau wa taasisi mbalimbali ili kukuza vipaji vyao.
Mechi hizi za kirafiki ni kati ya michezo ambayo husaidia jamii kukutana kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri na vile vile husaidia kuhamasisha vijana kufanya mazoezi katika kuunga mkono kampeni ya serikali ya kufanya mazoezi katika jamii ili kujiepusha na hatari ya kupata magonjwa yasioambukizwa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...