Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo Jumatano, Mei 24, 2017 ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Ndg John Lipesi Kayombo kuanza mchakato wa ukamilisho wa ujenzi wa Madarasa manne katika shule ya Sekondari Mburahati iliyopo Katika Mtaa wa Barafu, Kata ya Mburahati Jijini Dar es salaam.

Sambamba na Agizo hilo pia ameagiza kujengwa vyoo vya wanafunzi kutokana na uchache wa vyoo vilivyopo ili kukabiliana na wingi wa wanafunzi.

Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo wakati wa kikao Cha pamoja kilichofanyika Shuleni hapo kwa kuhudhuriwa na Uongozi wa Shule hiyo, Kamati ya Shule, Uongozi wa serikali ya Mtaa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Mburahati.

Mhe Makori alisema kuwa kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na kidato Cha kwanza Kila mwaka kumekuwa na upungufu mkubwa wa madawati Jambo ambalo linachangia wanafunzi shuleni hapo kuanza kusoma kwa kupokezana hivyo mpango mahususi kukabiliana na changamoto hiyo ni pamoja na kuanza kujenga miundombinu ya kutosha itakayowasaidia wanafunzi kupata elimu bora.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika shule ya Sekondari Mburahati iliyopo Katika Mtaa wa Barafu, Kata ya Mburahati Jijini Dar es salaam.Leo Jumatano, Mei 24, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisikiliza maelezo kuhusu shule ya Sekondari Mburahati mara baada ya kuzuru shuleni hapo.Leo Jumatano, Mei 24, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kulia) akimsikiliza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mburahati Ndg Bagaya Kashato akitoa maelezo kuhusu  kukwama kwa ujenzi wa madara ya shule ya Sekondari Mburahati mara baada ya kuzuru shuleni hapo, Mwingine ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James mkubo.Leo Jumatano, Mei 24, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...