Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa imepongezwa kwa kusimamia vyema Sheria na
Kanuni zinazoongoza vyama vya Siasa hapa nchini hali inayochochea kukua
kwa demokrasia.
Akizungumza katika mkutano wa kawaida wa siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa, Katibu Mkuu wa Chama cha UDP Dkt. Goodluck Ole Medeye amesema utaratibu wa kuvisimamia vyama na kuvikagua ili kuhakikisha kuwa vinazingatia Sheria na Kanuni ni mzuri na ni wa kupongezwa.
“Napongeza kwa kazi nzuri ya kukagua hesabu za vyama inayofanywa na mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa vyama vinavyopata ruzuku na visivyopata ruzuku hali ambayo inachochea uwajibikaji katika vyama ” alisisitiza Ole Medeye.
Akifafanua Ole Medeye amesema kuwa Serikali kupitia Msajili wa vyama vya Siasa anafanya kazi nzuri ya kuhakikisha kuwa kila chama kinafuata taratibu na kuomba ofisi hiyo kuendeleza utaratibu wa kukutana na viongozi wa vyama na wale wanaosimamia rasilimali za vyama kwa lengola kuhakikisha kila kimoja kinatimiza na kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa na watendaji wao wakati wa mkutano wa siku moja uliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kujadili na kuweka mikakati ya kuondoa mapungufu yanayojitokeza katika kutekeleza Sheria na Kanuni za usajili wa vyama vya Siasa hapa nchini. Kushoto ni Msajili Msaidizi Bw. Sisty Nyahoza na kulia ni Msajili Msaidizi Bi. Piencia Kiure.
Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akisisitiza jambo kwa viongozi wa vyama vya Siasa (hawapo pichani),wakati wa mkutano wa siku moja na viongozi hao leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msajili Msaidizi Bw. Sisty Nyahoza.

Msajili Msaidizi Bw. Sisty Nyahoza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayovihusu vyama vya siasa ikiwemo utekelzaji wa Sheria namba 5 ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992.

Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha CCK Bw. Renatus Muhabi mara baada ya kumaliza mkutano wa siku moja uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu ulioanzishwa na Msajili wa vyama vya siasa kukutana na viongozi wa vyama hivyo na watendaji wao.

Katibu Mkuu wa Chama cha UDP Goodluck Ole Medeye akipongeza utaratibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa kusimamia sheria na kanuni zinazosimamia vyama vya siasa ikiwemo kufanyika kwa ukaguzi wa mahesabu katika vyama vyao.(Picha na Frank Mvungi-Maelezo).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...