Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta  Ndetiye (kushoto) akizungumza wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na kufanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe. Semina hiyo ilihusu umuhimu wa uhifadhi wa Maliasili Malikale na Maendeleo ya Utalii nchini.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muda mfupi kabla ya kuanza kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika semina hiyo. Mada zilizowasilishwa katika semina hiyo ni Kwanini Watanzania tuhifadhi uoto wa asili na Wanyamapori, Athari za Muingiliano wa Mifugo na Wanyamapori, Maendeleo ya Utalii na umuhimu wake katika uchumi wa Tanzania na Umuhimu wa Uhifadhi wa Misitu Nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jeneral Gaudence Milanzi akizungumza katika semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Idara wa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexander Songorwa askiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Watanzania kuhifadhi uoto wa asili na Wanyamapori katika semina hiyo. Kushoto waliokaa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya viongozi na wakurugenzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naona kama Makumbsho ya Taifa imeachwa nyuma sana katika wizara hii, sijaona msemaji wa Taasisi hii Muhimu sana kwa Taifa hili. Si vyema Taasisi hii ikasemewa na Idara nyingine zilizopo katika wizara maana nayo inaumuhimu wake Mkubwa sana kwa Taifa hili. Ni mtazamo wangu tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...