Makampuni ya Tanzania ya uwakala wa usambazaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi, wameshauriwa kuyashawishi makampuni ya nje kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hapa hapa nchini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam wakati akitembelea mabanda ya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Akifuatana na Mkurugenzi wa TPSF Bw. Louis Accaro, Afisa Biashara wa Tan-Trade Bw. Mohamed Mkadara, na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wajasiriamali Bi. Jacquiline Maleko, Dr Mengi ametembelea mabanda mbalimbali, yakiwemo yaliyopo chini ya mwamvuli wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda, na Kilimo – TCCIA, Mfuko wa Fursa sawa kwa wote-EOTF, na Banda la Kampuni ya Agricom, ambayo Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Angelina Ngalula alielezea jinsi ilivyojipanga kusambaza zana za kisasa za kilimo ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji. Katika majumuisho yake Dr Mengi alishauri Tan-Trade na TPSF washirikiane katika kuangalia namna ya kuboresha zaidi maonyesho hayo, hususan katika kuboresha mabanda ya maonyesho ili yalingane na hadhi halisi ya kimataifa.

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...