Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Profesa Ibrahim Hamisi Juma, (kushoto),
akikaribishwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia Kwa
Wafanyakazi, (WCF), Bw. Sebera Fulgence, alipotembela banda hilo kwenye
hema la Jakaya Kikwete viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama
Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho
ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam Julai 4, 2017. Mhe
Profesa Hamisi alitumia kwa uchache dakika 15 akiwa na shauku ya kupata
taarifa zaidi kuhusu kazi na majukumu ya Mfuko huo.
Mhe Profesa Hamisi alielezwa kuwa Mfuo huo umeundwa mahsusi kwa ajili ya kutoa fidia stahiki kwa Mfanyakazi aliyepata ugojnwa au kuumia mahala pa kazi. Hali kadhalika, alielezwa kuwa pamoja na kwamba Mfuko huo ni wa Hifadhi ya Jamii, namna ya uchangiaji wake unatofautiana na Mifuko mingine, ambapo Mwajiri ndiye anawajibika kisheria kumchangia mfanyakazi wake kila mwezi wakati Mifuko mingine, wachangiaji ni wote, mwajiri na mwajiriwa.
Wakati hyuo huo, Waziri anayehusika na sekta ya Viwanda na Biashara, sekta ambayo inatoa ajira kubwa kwa wafanyakazi, naye alipata fursa ya kutembelea banda hilo ambapo kama ilivyokuwa kwa Kaimu Jaji Mkuu naye alielezwa majukumu yanayotekelezwa na Mfuko ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Sebera Fulgence, alimueleza kuwa sekta ya viwanda na biashara ni miongoni mwa sekta zinazotoa wanachama wengi kwenye Mfuko huo, ukiachilia elimu na afya na kwamba Mfuko umekuwa ukiendelea kutoa elimu zaidi kwa waajiri kuhusu umuhimu wa kuchangia wafanyakazi wao kwa manufaa ya mwajiri na mwajiriwa pindi yanapotokea madhara.
Mfuko wa WCF ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi (sura 263 marejeo ya mwaka 2015).

Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence(kulia), akimpatia
maeelzo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma
(kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera
Fulgence(kulia), akimpatia maelezo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli
zifanywazo na WCF.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kulia), akizungumza
jambo na Maafisa wa WCF, Bw. Sebera Fulgence (wapili kushoto) ambaye ni
Afisa Uhusiano Mwandamizi na Bi.Bi.Inocencia William
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...