Na Karama Kenyunko,Glogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo mapema imeelezwa kuwa jalada la kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya aliyekiwa Mkurugenzi Mkuu Wa Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu,  lipo kwa DPP.

Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali, Peter Vitalis ameeleza hayo mbelw ya Hakimu Mkazi Respicius Mwijage.

Amedai kuwa shauri hilo leo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini jalada halisi la kesi hiyo liko kwa DPP na pia upelelezi bado haujakamilika, hivyo likirejeshwa ndipo itafahamika upelelezi umefikia wapi.

Hata hivyo, Hakimu Mwijage amesema kesi hiyo ina mwaka mmoja na upelelezi haujakamilika, hivyo wakamilishe ambapo  ameahirishwa kesi hadi September 28/2017.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa Maimu na wenzake, wanakabiliwana mashtaka ya 27 yakiwemo ya kutumia madaraka vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh 1,169,352,931.

Mbali ya Maimu, washtakiwa wengine  Ni aliyekiwa Meneja Biashara Wa NIDA, Avelin Momburi, Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani. Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji,  George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond naXavery Kayombo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...