Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.
UPANDE wa utetezi umeiomba Mahakama kuulazimisha upande wa mashtaka kuifuta kesi ya utakatishaji fedha, inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake.

Wakili wa utetezi, Majura Magafu ametoa ombi hilo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mbele ya Hakimu Mfawidhi Cyprian Mkeha wakati kesii hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Ameiomba mahakama kuwa, upande wa mashtaka ulazimishwe kesi ifutwe ama waiondoe mahakamani kwa sababu washtakiwa awali walikuwa chini ya dhamana na wakiripoti kila walipohitajika Takukuru.
Amesema,
Wakili wa utetezi, Majula Magafu amedai kuwa sasa imefikia wakati mahakama ihakikishe maelekezo inayoyatoa yanaheshimiwa

"Mahakama inaweza kuifuta kesi ili ushahidi ukikamilika waletwe tena, kwa sababu imebaki hadithi kila wakija wanasema wanasubiri vielelezo kutoka Ulaya na miaka inaenda tu,".

Akijibu hayo, wakili wa serikali, Constantine Kakula amedai upelelezi wa kesi hiyo unashindwa kukamilika kwa sababu inahusisha uchunguzi unaovuka mipaka.

Amedai, siyo kama jamhuri imelala bali inafanya mawasiliano na upande wa pili, kwa sababu hatuwezi kumlazimisha anayetuma nyaraka za upelelezi kutoka Ulaya.

Hakimu Mkeha akautaka upande wa mashtaka kuhakikisha unakamilisha upelelezi.

 Kitilya na wenzake, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na Sioi Solomon wanashtakiwa kwa utakatishaji wa fedha dola milioni 6.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi September 8/2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...