Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
MFANYABIASHARA Ramadhani Athumani Juma maarufu kama Elias Jeremiah Mazimbaka amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la kujifanya kuwa yeye ni Mkurugenzi wa Habari wa Ikulu, Gerson Msigwa.(Pichani Chini)
Akisoma hati ya mashtaka leo mapema, wakili wa Serikali, Jackline Nyantori amedai, kati ya Juni 28 na Julai 4, mwaka huu jijini Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya mtuhumiwa huyo alijitambulisha kwa mtu mmoja anayeitwa Ladislous Matindi kuwa yeye ni Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa HABARI wa Ikulu.
Mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa imedaiwa, mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujaribu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mshtakiwa amekana mashtaka na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana mahakama ilimtaka kuwa na wadhamini wawili watakaoweka dhamana sh milioni moja
Kesi imeahirishwa hadi Agosti 23,mwaka huu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...