Na Bashir
Yakub.
Kuna matatizo sana
kati ya wapangaji
na wenye nyumba
kuhusu notisi ya
kuondoka au kuondolewa.
Wako wanaosema notisi
ni mwezi mmoja, wako
wanaosema ni miezi
mitatu n.k. Kama
ni kweli ama hapana
tutaona hapa sheria inasemaje.
Masuala ya pango
yanaongozwa na sheria
kuu mbili. Moja
sheria ya ardhi
namba 4 ya
mwaka 1999 na
pili sheria ya
mikataba sura ya
345. Kwa pamoja
sheria hizi mbili
husimamia jambo hili.
1.MIKATABA YA PANGO.
Mikataba ya pango
inahusisha makubaliano ya
upangaji kati ya
mwenye nyumba na
mpangaji au mpangaji
na mpangaji mwingine
wa pili. Pango
laweza kuwa la
nyumba ya kuishi,
kwa ajili ya biashara,
nyumba ya ibada
au shughuli nyinginezo.
Yote haya yataingia
katika maana ya
pango.
2. AINA
ZA MIKATABA YA
PANGO.
Sheria ya ardhi vifungu
vya 78 na
79 inatambua mikataba ya
upangaji ya muda
mrefu na vipindi
vifupi. Inatambua pango la
wiki, mwezi, miezi,
mwaka na miaka.
Imetoa uhuru kwa
wahusika wenyewe kuamua
ni muda gani
wangependa kuingia mkataba.
3. NOTISI
YA KUONDOKA.
Katika vitu muhimu
sana katika suala
la pango ni
notisi ya kuondoka au kuondolewa
katika pango. Jambo
la kuzingatia awali kabisa
ni kuwa notisi
hii ni muhimu
pande zote mbili.
Upande wa mwenye
nyumba na upande
wa mpangaji. Kila
mmoja kwa nafasi
yake anawajibika kutoa
notisi kwa mwenzake
panapo mahitaji ya
kuondoka au kuondolewa.
Ikumbukwe notisi si
kwa ajili tu ya
kuondoka na kuondolewa bali
pia hutakiwa yanapotokea mabadiliko yoyote
katika masharti ya
mkataba. Hii ina maana
hata kuongeza kodi, kupanga
kukagua nyumba, kufanya marekebisho
n.k. notisi yafaa
itolewe.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...