Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo leo tarehe 24 Agosti, 2017 amefanya kikao cha kazi na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO mkoa wa Mtwara mjini Mtwara lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto za utendaji kazi. Dkt. Pallangyo amewataka watendaji hao kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa mapato pamoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji za kila baada ya miezi mitatu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele) akiongoza kikao
kilichoshirikisha watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya
Kusini na Ofisi za TANESCO mkoa wa Mtwara mjini Mtwara
Sehemu ya watendaji kutoka
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO- Mtwara
wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika
kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akisisitiza jambo katika
kikao hicho
Afisa Rasilimaliwatu wa Kanda
ya Kusini, Bonus Msuha (kushoto) akieleza jambo katika kikao hicho. Kulia ni Meneja
wa TANESCO-Mtwara Mhandisi Aziz Salum
Sehemu ya watendaji kutoka
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO- Mtwara
na Wizara ya Nishati na Madini
wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo
pichani) katika kikao hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...