
Na Hussein Mohamed Bashe
Mbunge
Jimbo la Nzega Mjini, Tabora.
Mapema Januari mwaka huu nilipata nafasi ya kushirikiana na wananchi katika kazi za maendeleo Jimboni kwangu Nzega Mjini katika Kata ya Itilo ambapo nilikuwa na kazi ya kuhamasisha na kusaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Itilo.
Nikiwa katika eneo hilo nilipata nafasi ya kukutana na mtoto mchangamfu ambaye anaitwa Suzan.
Bahati nzuri ni kuwa Suzan alikuwa akisoma katika shule hiyo katika madarasa ya Awali, nilimkuta amekaa chini na wenzake.Suzan ni mtoto anayejiamini na huenda shule kila siku, waalimu wake walinambia Suzan huwa hakosi kwenda shule na hana udhuru wa mara kwa mara kama watoto wengine.
Nilivutiwa sana na habari za Suzan na tabia yake ya kupenda shule hivyo tukaamua kwa pamoja na wananchi kuanza mchakato wa ujenzi wa madarasa na sasa tumeyamaliza na nimekwisha kuyakabidhi kwa Shule na wananchi wa Itilo.
Wiki hii nimefika tena Jimboni nimekutana na Suzan kwa mara nyingine; na nimepata nafasi ya kuongea naye zaidi; Suzan ameniambia anataka siku moja kuwa Mbunge kama mimi na anapenda namna ninavyowapenda watoto.Uwezo mkubwa na kujiamini kwa Suzan kunanipa faraja kuwa naye karibu zaidi na kumsaidia zaidi.
Kwa sababu yake nilisukumwa kujenga madarasa mengine mawili zaidi katika Shule ya Msingi Itilo ili kuwajengea watoto wetu mazingira mazuri ya kujifunza.
Nimemuomba Mwenyezi Mungu anipe nguvu na uwezo niendelee kumsaidia, kumlinda na kumtunza Suzan siku zote mpaka aakapotimiza ndoto zake siku moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...