Na Tiganya Vincent.

SERIKALI Mkoa wa Tabora imeagiza kutafutwa na kuchukiwa hatua kali na kupata maelezo ya watu waliohusika na uchomaji moto katika maeneo ya Chuo cha Ardhi Tabora na kusababisha uharibifu mkubwa wa mistu asili na miti iliyokuwa imepandwa katika eneo hilo kama hatua za uhifadhi wa mazingira.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri baada ya kukuta eneo la Chuo hicho likiwa limeungua na moto wakati wa ziara ya ya kukagua vitalu vya kuoteshea miti ikiwa ni maandilizi ya zoezi la upandaji wa miti.

Alisema kuwa haiwezekani wananchi wanajitoa kwa moyo kupanda miti katika kampeni inayoendelea kisha watu wachache wanaamua kuua miti na kuharibu mazingira.

Mwanri aliongeza kuwa inasikitisha kuona hata sehemu za Taasisi za umma kama hiyo zinaacha moto unaunguza miti na wakufunzi wapo, wanachuo wapo bila kuchukua hatua ya kuuzima na kuwasaka waliohusika.

Alisema kitendo kinaonyesha jinsi wao nao wanahusika kwa namna moja au nyingine katika kuchangia uharibifu ulifanyika katika Chuo chako.
Kufuatia kitecho hicho Mkuu wa Mkoa alimwagiza Afisa Mazingira wa Manispaa ya Tabora kwenda kwa Mkuu wa Chuo kupata maelezo nini kilitokea na hatua zilizochukuliwa kwa wahusika na kama hawachukua hatua kwa wahusika basi Sheria za Mazingira zichukue mkondo wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...