Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Cosmas Cheka amekata rufaa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupinga matokeo na adhabu ya kufungiwa miezi sita na faini ya Sh200,000 iliyotangazwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).

Cheka alisema hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa TPBC ilikuwa na njama dhidi yake ili kumtengenezea nafasi bondia Haidary Mchanjo katika ngumi za kulipwa nchini.

Alifafanua kuwa adhabu dhidi yake haikufuata sheria kwani kwanza hakupewa nafasi ya kusikilizwa kwa mujibu wa sheria, huku akimpa nafasi mwamuzi wa pambano hilo, Modest Rashid ambaye alitaka kupigana naye kuitwa na kujieleza katika kikao cha TPBC.

“Hata kwenye mahakama, lazima mtuhumiwa apewe nafasi ya kusikilizwa au kujitetea, mimi nilikuwa ulingoni na mwamuzi na mpinzani wangu Mchanjo, mwamuzi amenitolea maneno machafu sana, haikutosha akaamua kunikata pointi, niliandika barua ya kulalamika TPBC, hawajaniita na kuibuka na adhabu kwangu,” alisema Cheka.

Alisema kuwa pamoja na maamuzi hayo kutonifikia kimaandishi, nimeamua kuchukua hatua za haraka kwani tayari vyombo vya habari mbalimbali na mitandaa ya kijamii yamekwisha tangaza maamuzi hayo yaliyofanywa bila kufuata sheria kwani hawakunipa nafasi ya kusikilizwa kwa mujibu wa sheria. 


Meneja wa bondia wa Cosmass Cheka, Juma Ndambile (kulia) akizungumzia matatizo yaliyompata bondia wake. 
Cosmass Cheka akizungumzia hatua aliyochukuwa ya kukata rufaa BMT kupinga kufungiwa na matokeo ya pambano lake dhidi ya bondia Haidary Mchanjo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...