Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio anasikitika kutangaza kifo cha Mjumbe wa Bodi ya PPF Bwana Nassor Baraza kilichotokea jana tarehe 14/08/2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Jijini Dar es salaam.
Msiba upo nyumbani kwa Marehemu, Mikocheni Regent Estate Namba 25 karibu na shule ya Sunrise au nyuma ya jengo la GEPF. Mazishi yanafanyika leo tarehe 15/08/2017 katika makaburi ya Kisutu saa kumi jioni.
Innah Lillah Wainnailaih Rajiun
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...