Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kushoto) alipokuwa akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari ya Chokocho Wilaya ya Mkoani lenye madarasa manne na Chumba cha Maabara leo akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba (kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoku wa akiuliza suala na kutoa maelekezo kwa Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Chokocho Maalim Abdalla Mohamed Abdalla (kushoto) wakati alipoikagua maabara katika skuli hiyobaada ya kuifungua rasmi pamoja na madarasa manne ya kusomea (kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma,Rais akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Chokocho Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ili kuzungumza na Wazee,Wananchi hao pamoja na Walimu katika uzinduzi wa jengo la madarasa manne (4) na Chumba cha maabara leo katika Skuli ya Sekondari ya Chokocho akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...