Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau amewasilisha Hati za Utambulisho (Letters of Credence) kwa Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo katika sherehe zilizofanyika siku ya Jumanne ya tarehe 12 Septemba 2017 katika Ikulu ya Indonesia maarufu kama Istana Maderka.
Kuwasilishwa kwa Hati hizo kunatoa ruksa wa Balozi Dkt. Dau sasa ya kufanya shughuli za uwakilishi nchini Indonesia kwa uhuru pasipo kuvunja taratibu za Kidiplomasia.
Imetolewa na:
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kuala Lumpur
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akiwasili katika Ikulu ya Indonesia maarufu kama Istana Maderka tayari kuwasilisha Hati za Utambulisho (Letters of Credence) kwa Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo
 |
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akiwasilisha Hati za Utambulisho (Letters of Credence) kwa Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo |
 |
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akipeana mikono na Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho (Letters of Credence) |
 |
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akiongea na Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. |
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi jijini Kuala Lumpur Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau akiagana na Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...