Benki ya CRDB leo imekutana na wafanyabiashara wadogo na wa kati mkoani Mwanza na kuwahakikishia kwamba itaendelea kutoa huduma bora ikiwemo mikopo ili kukuza mitaji yao.

Akisoma hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt.Charles Kimei, Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba huduma za mikopo zitatolewa kwa wakati wote katika benki hiyo kwa kuzingatia kanuni za kibenki nchini.

Amesema benki hiyo imeendelea kutanua na kuboresha huduma zake ikiwemo uwepo wa Matawi 20, vituo vya kutolea huduma 50, ATM 135, mawakala wa Fahari huduma zaidi ya 649 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Aidha amesema kwa mkoa wa Mwanza benki ya CRDB ina matawi manne, vituo vya huduma 13 pamoja na Mawakala wa Fahari Huduma zaidi ya 105 na hivyo kusaidia kuwafikia wateja wake kwa urahisi.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo, Agapiti Malya pamoja na Doroth Baltazari wameipongeza benki hiyo kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.
Baadhi ya wafanyabiashara (wajasiriamali) wadogo na wa kati walioshiriki mkutano ulioandaliwa na benki ya CRDB mkoani Mwanza kwa ajili ya kujadili pamoja masuala mbalimbali ya kibenki ili kusaidia kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoani Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huu, hii leo Jijini Mwanza
Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada kwenye mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...