Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (wapili kulia), akizungumza na Ma IGP
wastaafu na makamishna wastaafu na waliopo kazini (hawapo pichani) wakati alipokutana
nao leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mpango wa kubadilishana uzoefu wa kikazi
pamoja na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya
uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo,
kulia ni IGP mstaafu Said Mwema, wa kwanza kushoto ni IGP msataafu Ernest Mangu
na IGP mstaafu Omari Mahita.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Mstaafu (IGP) Ernest Mangu (kushoto), akizungumza mbele ya makamishna wastaafu
na waliopo kazini (hawapo pichani), kwenye kikazo kazi kilichoandaliwa na Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (wapili kulia) kwa lengo la kubadilishana
uzoefu na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya
uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi hilo leo
jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni IGP msataafu Said Mwema na wapili kulia
ni IGP msataafu Omari Mahita.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Mstaafu (IGP) Omari Mahita (wapili kushoto), akizungumza mbele ya makamishna
wastaafu na waliopo kazini (hawapo pichani), kwenye kikazo kazi kilichoandaliwa
na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (wapili kulia) kwa lengo la
kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na matishio
mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa
Jeshi hilo leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni IGP msataafu Said Mwema na
kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu (IGP) Ernest Mangu.
Kamishna wa Utawala ndani
ya Jeshi la Polisi DCP Leonard Paul (aliyesimama), akiwasilisha mada mbele ya
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro na ma IGP wastaafu na Makamishna
wastaafu wa Jeshi hilo na waliopo kazini, kwenye kikazo kazi kilichoandaliwa na
Mkuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kupeana mbinu na mikakati
ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya kuboresha utendaji wa
Jeshi hilo leo jijini Dar es salaam.
Ma IGP na Makamishna wa
Polisi wastaafu na waliopo kazini wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi hilo (IGP) Simon
Sirro, wakati alipokutananao leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mpango wa
kubadilishana uzoefu wa kikazi pamoja na kupeana mbinu na mikakati ya
kukabiliana na matishio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu pamoja na mikakati ya
kuboresha utendaji wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...