Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Wakili wa serikali, Paul Kadushi ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage. Wakati shauri hilo lilipokuja kwa kutajwa na kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
UPANDE wa Mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni mbili, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) umeieleza mahakama kuwa, sehemu kubwa ya upeleleIezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika.
Aidha wamedai kuwa wako kwenye majadiliano kuona kama wataongeza washtakiwa wengine au la.

Aidha upande wa utetezi umeileza mahakama kuwa wamewasilisha maombi ya dhamana katika mahakama kuu divesheni ya rushwa na uhujumu uchumi “mahakama ya mafisadi”.
Pia wameiomba mahakama tarehe itakayofuata upande wa mashtaka uje ueleze hatua ya upelelezi ilipofikia.
Pia wameiomba mahakama tarehe itakayofuata upande wa mashtaka uje ueleze hatua ya upelelezi ilipofikia.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 12 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...